MULEMBE WAUNGANE NDIPO WAPATE URAIS KWA URAHISI
Jamii ya Mulembe iliyo ya pili kwa idadi kubwa nchini, imejipata katika njia panda kisiasa tarehe ya uchaguzi mkuu inapokaribia.
Hii inatokana na hali kwamba wanasiasa kutoka jamii hii kugawika katika vyama mbalimbali. Hawazungumzi kwa usemi mmoja ikizingatiwa wana ndoto ya kuingia ikulu.
Kulingana na sensa mwaka wa 2019, idadi kabila la Mulembe ni takribani milioni saba.
Kwa msingi wa idadi ya wapigakura jamii hii ina jumla ya wapigakura karibu milioni nne wakiwemo wale walio nchini na maeneo mengine ya Kenya.
Kwa hivyo ninaamini kuwa ikiwa viongozi hawa wataongea kwa usemi mmoja kisiasa,bila shaka wana uwezo wa kupata kiti cha urais.
Comments
Post a Comment